1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal yapania kutwaa ubingwa

5 Februari 2024

Arsenal ilirejesha azma yao ya kunyakua taji la kwanza la Ligi ya Premia katika kipindi cha miaka 20 kwa kuwalaza viongozi wa ligi Liverpool 3-1 huko ndani ya uga wa Emirates.

https://p.dw.com/p/4c4Ur
Mikel Arteta
Kocha wa Arsenal Mikel ArtetaPicha: Kirsty Wigglesworth/AP Photo/picture alliance

Chelsea waliangukia kipigo kingine cha aibu, 4-2 nyumbani dhidi ya Wolves, jana Jumapili.

Matumaini ya Liverpool kumuaga kocha Klopp Jugen Klopp kama bingwa wa England yanafifia wakati Arsenal ikipunguza mwanya wa hadi pointi mbili kwenye jedwali.

Soma pia: Arsenal kufanya usajili muhimu ili kuikabili Man City

Mikel Artetaalikiri kabla ya mchezo kwamba timu yake haikupaswi kurudia kipigo cha 2-0 cha Kombe la FA dhidi ya Liverpool mwezi uliopita ikiwa wangetaka kuweka hai matumaini yao ya ubingwa.

Mabingwa watetezi Manchester City wamesalia na pointi tano tu kutoka kileleni wakiwa na mechi mbili za ziada, wakianza na ziara ya Brentford leo Jumatatu.

Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino aliwaomba radhi mashabiki wa Chelsea baada ya hat-trick ya Matheus Cunha kuipa Wolves ushindi wa kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge tangu 1979. The Blues walizomewa na mashabiki waliokuwa na hasira baada ya kushuka hadi nafasi ya 11 wakiwa na jumla ya pointi 31.

Kwengineko Mashetani wekundu, Manchester United walipanda hadi nafasi ya 6 kwenye jedwali baada ya kuilaza 3-0 West Ham. Wachezaji Rasmus Hojlund na Alejandro Garnacho walingara katika mechi hiyo.