1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolsonaro arejea nyumbani Brazil kuuongoza upinzani

Bruce Amani
30 Machi 2023

Rais wa zamani wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Brazil Jair Bolsonaro amerejea nyumbani leo baada ya kuishi kwa miezi mitatu jimboni Florida, Marekani.

https://p.dw.com/p/4PW9D
Brasilien Jair Bolsonaro Ankunft
Picha: REUTERS

Balsonaro alikaribishwa na mamia ya wafuasi wake katika uwanja wa ndege wa Brasilia kabla ya kuelekea moja kwa moja katika mikutano na chama chake cha kisiasa.

Bolsonaro, ambaye hakuwahi kukubali rasmi kushindwa katika uchaguzi wa mwaka jana, ameapa kuongoza upinzani dhidi ya serikali ya Rais wa siasa za mrengo wa kushoto Luiz Inacio Lula da Silva.

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro arejea Brazil baada ya kukaa Florida, Marekani kwa miezi mitatu

Bolsonaro alikimbilia Marekani, siku mbili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Lula mnamo Januari mosi.

Alisema alihitaji kupumzika, lakini wakosoaji wanasema alikuwa anakwepa hatari ya kufanyiwa uchunguzi wa kisheria wa kesi kadhaa ambazo huenda akakabiliwa nazo nchini Brazil.